Social Icons

Pages

Tuesday, May 13, 2014

Malimwengu Mazito

Lulu:

Mbona umeshika tama, wajihi umeukunja?
Na mawazo wayakama, furahayo meivunja.
Kwenye sikitiko hama, we Hamadi wajipunja.
Siha yako 'taichoma, ukauke kama kanja.

Mchokozy:
Bahati sinayo jama, sijakufuru mizanja.
Maisha yamenifuma, Lulu sinao ujanja.
Upande huu meinama, malimwengu yanichanja.
Pande ile nalalama, walimwengu wanibanja.

Lulu:
Maisha kama mashua, leo kesho yaweza zama.
Si mchezo wa kwachua, kuibukia au kuzama.
Kosea kuyafumbua, utape ukiita mama.
Dunia imechanua, Mungu ameumba tizama.

Mchokozy:
Ulimwengu kuchanua, sikatai naungama.
Ela kwa walo kwachua, wakajishindia bima.
Mie seshi kujifua, Kwangu mie ni mlima.
Madini sijayazua, wala siwezi kuulima.

Lulu:
Ugomvi wataumwaya, suluhisho kwao vita.
Wanyonge watapwaya, kuonewa wanapopita.
Ulimwengu sio m'baya, haki ilikwishakita.
Binadamu ndio wabaya, kwelekeza yetu dira.

Mchokozy:
Nitafikwaje mimi tu? wengi wana afadhali.
Sitangamani na watu, idhaifu yangu hali.
Kwao mimi ni kiatu, sina hali wala bali.
Si thamani mie jitu, ardhi si pangu pahali.

Lulu:
Tazama mpaka mwisho, dunia wakaribio.
Ishara nahiri tokeo, kama tukufu maandiko.
Hamna ataye bakio, sio petu pahalipo.
Lazima yote matimio, kwetu yawe mazito.

Mchokozy:
Maandiko nayaamini, hatubaki duniani.
Fikra ilo akilini, tangulio kuzimuni.
Hamadi sina sinani, wa kuniauni simwoni.
Maswahiba kwaherini, dunia nawaachieni.

By Princesslumy Lulu and Mshairi Mshari.


No comments:

Post a Comment