Social Icons

Pages

Tuesday, May 13, 2014

Maendeleo - Kilimo vs Tekelinalokujia


Nyie mwasema kilimo,Eti uti wa mgongo
Mbona nyie hamumo,Au mwasema uongo?
Mme yawacha mashimo,Wasomi wenye mipango
Njooni kwenye kilimo,Acheni kubeba bango

Sasa kilimo ni uti wa mgomgo
wakati tekelinalokujia ndio somo
Mimi sibagua hata jembe nawezashika
Wasomi wenyewe ndo waendeleza kilomo mpango

Hilo tekelinalotujia,Limerushwa na kiatu
Vijijini lakimbia,Limefikia mjini tu
Masikini wanalia,Wamekauka watupu
Mali mmekumbatia,Sisi twasaga viatu

Mashule kufunguliwa teke kurushiwa vijijini
Wanafunzi kuwezeshwa kweli wataka iwe jiji
Maendeleo hupelekwa uliza izo charitizi
Kusema watu wachoyo sio wote duniani

Mengi nakuachia, kweli hili swala sila mmoja
Hamna wakumlaumu, tajiri anayake mawazo
Huwezi kumuukumu, ila kumbuka wale watoao
Hili swala la maendeleo ni jukumu letu sote.

Lulu Mero & Rashid Mohammed 

No comments:

Post a Comment